Mlinzi Michael Kibwage akishiriki moja wapo ya debi la mashemeji baina yao na Gor Mahia kuwania ligi kuu soka taifa Kenya. Picha/Kwa hisani
Mlinzi Michael Kibwage akishiriki moja wapo ya debi la mashemeji baina yao na Gor Mahia kuwania ligi kuu soka taifa Kenya. Picha/Kwa hisaniKlabu ya AFC Leopards imepigwa jeki pakubwa kuhusu mechi yao ya Jumapili hii dhidi ya Zoo Kericho kwenye ligi ya KPL, hii ni baada ya kurejea mazoezini kwa mlinzi Michael Kibwage aliyekuwa akiuguza jeraha.
Mlinnzi huyo alivuna jeraha la kisugudi kwenye mechi ya siku 10 zilizopita dhidi ya Tusker na kulazimisha kukosa kushiriki debi la mashemeji wiki moja iliyopita ila sasa yu kwenye hali shwari ya kucheza dhidi ya vijana wa kocha Sammy Okoth. 
Ronald Namai, afisa mkuu mtendaji wa Ingwee amethibitisha kurejea kw akijana huyo na kudai jeraha lake halikuwa bay asana ila kocha Matano ndiye atakayeamua kama atamtumia mara moja.
Leopards itawania kuvuna ushindi ili kuboresha nafais yake kwenye jedwali la ligi watakaposafiri Kericho ikitiliwa maanani timu zote mbili ziliandikisha sare ya 1-1 katika ngwe ya kwanza.


Post a Comment

Previous Post Next Post