Kikosi cha Harambee Stars chini ya miaka 21 kikiwa mazoezini uwanjani kasarani. Picha/Kwa hisani
Kikosi cha Harambee Stars chini ya miaka 21 kikiwa mazoezini uwanjani kasarani. Picha/Kwa hisani

Timu ya taifa ya soka Harambee Stars kwa washiriki chini ya miaka 21, imepata wakati mgumu wa kutonanili hata ushindi wowote kwenye ziara yao ya nchini Morocco kushiriki mechi za kujifua kwa kipute kijacho cha  CHAN mwakani, hii ni baada ya kushushiwa kipigo cha mabao 2-0 na wenyeji hao Morocco hapo jana.


Morocco walidhihirisha weledi wao wa kusakata ngozi ya ng’ombe iliyowambwa, kufumwa na kuundwa mpira kipindi cha kwanza ambapo mshambulizi wa Malaga Enes Syri alipata nafasi ya kukiramba kimia ila akafeli kuitumia vyema.


Goli la ufunguzi aidha lilitoka kwa Beelami Youssef dakika ya 69 kipindi cha pili kisha Hamza Hanouri akakomelea la ushindi dakika ya 80 huku Stars ikipotea kabisa mchezoni.


Kichapo hicho ni cha kwanza kwa vijana wa nyumbani kwa mechi mbili walizopiga kwenye taifa hilo la kaskazini mwa bara Afrika.


Timu hiyo inaongozwa na makocha Musa Otieno na Frank Ouna ambapo katika mechi ya kwanza dhidi ya Mauritania, ilisajili sare ya 1-1.
Post a Comment

Previous Post Next Post