Wachezaji wa AFC Leopards wakisherehekea goli walilofunga kwenye mechi ya ligi kuu KPL. Picha/Kwa hisani
Wachezaji wa AFC Leopards wakisherehekea goli walilofunga kwenye mechi ya ligi kuu KPL. Picha/Kwa hisani

Klabu ya AFC Leopards ilinyakua alama tatu muhimu jana jioni baada ya kuwanyuka wenyeji Thika united mabao 2-0, katika mechi ya kati kati mwa juma kuwania ligi kuu ya soka nchini KPL, ambayo iliandaliwa katika uwanja wa county ndogo ya thika.

Alex Kitenge aliiweka ingwe kifua mbele katika dakika ya 37, kabla ya Christopher Olum kujifunga mwenyewe kuipa leopards la pili. Ushindi huo unaipandisha ingwe hadi katika nafasi ya 11 na alama 31, kutokana na mechi 25 na unafufua matumaini ya kumaliza nane bora.

Uwanjani Kasarani, Masoud Juma aliifungia Kariobangi Sharks mabao mawili, na kuisaidia kunusuru sare ya kufungana mabao 2-2 na Posta Rangers, Joseph Nyaga pia aliifungia rangers mawili.


Na kule Mbaraki mjini mombasa, Tusker walivuna alama tatu baada ya kuinyuka Bandari, 3-0 Allan Wanga, Humphrey Mieno na Michael Khamati wakiifungia tusker

Post a Comment

Previous Post Next Post