Uga wa Kinoru ukikarabatiwa kwenye awamu ya kwanza. Picha/Martin Mwenda
Uga wa Kinoru ukikarabatiwa kwenye awamu ya kwanza. Picha/Martin Mwenda

Ukarabati wa awamu ya pili ya uwanja wa Kinoru mjini Meru kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya CHAN mwaka ujao nchini Kenya ulianza Jumamosi iliyopita, hii ni baada ya  maafisa wa kampuni ya Sports Kenya kupokea vifaa hitajika kutoka kwa seirikali kuu kwa ajili ya kazi hiyo.


Kwenye hafla ya kupokezwa vifaa hiyo, katibu mkuu katika wizara ya michezo Kirimi Kaberia alitangaza kwamba jumla ya shilingi milioni 892 zimetengewa kazi hiyo.Sisi kama serikali tuko hapa kuhakikisha tunatekeleza wajibu wa wito wa serikali ya Meru kukubali uga wa Kinoru utumiwe kwa mashindano ya CHAN.
Naamini Gavana na naibu wake pamoja nasi kama serikali tutashirikiana kuhakikisha tunakamilisha hili.
Kinoru ni moja wapo ya viwanja tutakavyotumia kwa CHAN na endapo utakamilika na kuafikia viwango hitajika basi hiyo itakuwa fahari kubwa kwetu.” Alinena Kaberia.Kwa upande wake, Gavana mpya wa Meru Kiraitu Murungi aliahidi kuwapa wanakandarasi uungwaji mkono kikamilifu kuhakikisha uga huo unaafiki viwango vya FIFA tayari kuandaa kipute hicho cha kihistoria.
Tunafurahia sana hatua ya serikali ya kitaifa kupitia kwa wizara ya michezo kukubali kufadhili ujenzi wa awamu ya pili ya uwanja huu wa Kinoru ili uafikie hadhi ya kimataifa.
Pia ningependa kuishukuru Kampuni ya Sports Kenya kwa kuchagua Meru kama moja wapo ya miji andalizi ya kipute cha CHAN mwakani.
Sports Kenya wamesema watafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha uwanja unakamilika kwa wakati ufaao.
Ni fahari kuona mataifa mbali mbali ya Afrika yakipiga kambi Meru kwa ajili ya kusakata dimba na wageni pia watakuwepo kwa wengi.
Baada ya michuano hiyo ya CHAN serikali ya kitaifa itarejesha uga huo kwa serikali ya kaunti ya Meru.” Aliongezea Gavana Kiraitu.”
Uga wa Kinoru ni moja wapo ya njanya tano zinazotarajiwa kuandaa dimba hilo pamoja na ule wa Kenyatta stadium mjini  Machakos, Moi International Sports Centre Kasarani na Nyayo hapa Nairobi, sawa na ule wa  Kipchoge Keino ulioko  Eldoret. Herbert Mwachiro ni naibu afisa mkuu mtendaji na mkurugenzi wa kamati andalizi ya CHAN humu nchini.
Moja wapo ya kazi zitakazofanyiwa uga huu ni pamoja na kubaidlisha nyasi zilizopo. 

Sura za uwanja huu zitakuwa sawa na zile zitakazotumika kwenye kombe la dunia nchini Urusi mwaka ujao.

Kuongezea, kutakuwa na taa za viwango vya juu,mbinu bora za mziki, runinga kubwa zitakazozingira uwanja sawa na nafasi za kukalia.
Ukarabati huo aidha unajiri siku moja tu baada ya shirikisho la soka barani Afrika CAF kupiga breki ukaguzi wake uliotarajiwa kufanyika Alhamisi ya Septemba 7 mwaka huu kuhusiana na maandalizi ya kipute hicho cha kuanzia mwezi Januari hadi Februari.Hatua hiyo imetokana na hali ilivyo ya kisiasa nchini, baada ya mahakama ya kilele kubatilisha ushindi wa Rais Uhuru Kneyatta kwenye uchaguzi mkuu uliopita wa Agosti 8.Akithibitisha haya, Rais wa shriikisho la soka nchini FKF Nick Mwendwa alidai kutokana na hatua hiyo, CAF imetuma naibu Rais wake  Constant Omari Selemani  kutathmini hali ya siasa nchini kabla ya kuendelea na ukaguzi wa viwanja. Caf imesema itatangaza tarehe mpya ya ukaguzi huo baada ya kupiga darubini joto la kisiasa nchini.Uamuzi wa kurejea tena debeni kumchagua rais wa tano wa Kenya sawa na kuhairishwa kwa ukaguzi wa viwanja kwa ajili ya maandalizi ya kipute cha CHAN unazidi kudidimiza imani ya dimba hilo kufanyika nchini kwani Kenya iko mbali sana na maadalizi huku kukiwa na ripoti kwamba CAF imetengea mataifa mawili kuchukua fursa hiyo endapo mpango wa Kenya utafeli.
Post a Comment

Previous Post Next Post