Katika hulka moja yapo ya binadamu katika maisha yake, kiashiria kinachoitwa kisingizio huwa hakikosekani. Na kwakawaida huwa kinajikita katikati ya nyakati ngumu zakimaisha haswa shida zinapomukumba binadamu. Hata katika kumbukumbu za vitabu vya dini, Mwanamme wa kwanza duniani Adamu alipoona amefanya makosa, hakuweza kukubali makosa yake kwa haraka ila alichokifanya pale Mwenyezi Mungu alipomuuliza kwanini ametenda dhambi, alijibu siyeye aliyetenda dhambi ila niyule mwanamke aliyemleta kama msaidizi ndiye aliyechangia afanye hivyo.

Dogo RIcie/Amz| Photo| Changez Ndzai

Dogo Richie Na Amz ProducerAmz producer nikati ya wataarishi wa muziki wazuri sana hapa mkoani Pwani, heshima yake na weledi katika tasnia nzima ya utayarishaji wa muziki ni ya haiba yake ya kivyake, kongole kwa hili. Hivyo kusema kweli mtu maarufu na muadilifu katika sanaa ya muziki kama yeye si shida kutengeneza mkwanja mrefu kupitia mikono yake kila siku. Mbali na kuwa amekuwa akifanya kazi za wasanii wakubwa wa Pwani, yeye pia nikioo na tamanio la vijana wengi wanaopania kuwa watawarishi wa muziki ziku za usoni. Hivyo nilazima wadau mbalimbali kwenye uga huu wa burudani, kutaka kujumuika ama kuwa karibu na star kwenye muziki kama yeye. Ila shida moja ya star huyu inawezekana kuwa hajawa mwepesi wa kuwekeza kwenye biashara yake vizuri, ama hata katika biashara nyingine mbali na muziki ilikujiweaka pazuri zaidi kwenye maisha yake.

Nasema hivi nikwakutokana na kauli yake ya leo asubuhi, Amz anavyolalama kuwa bishara yake ya muziki inaporomoka kisa na maana msanii Dogo Richie, ambaye anadai kuwa huwa anawatongoza wasanii haswa wa kike kwa kisingizio kuwa atawasaidia kuwainua kimuziki. Amz kama Producer mkubwa, amelitumbua jipu na kulijibu swali kwanini Sanaa ya muziki Pwani inauhaba wa wasanii wa kike na kwanini wale kidogo waliopo pia nivigumu kuwaona waking'ara kwa sana. Kama mdau kwenye tasinia hii, sitasema wala sitaki kuegemea upande wowote ule (Upande wa Richie ama Amz)  ila huenda kama kweli Dogo Richie ameshawahi kufanya hivyo basi mara hii amemumegea tunda lake Producer Amz. Uchungu wakupokonywa mpenzi, ama kupokonywa nyama mdomoni kwa lugha ya mtaani, huwa unauma sana. Nakama nilivyotangulia kusema basi Amz ameona yakwamba niheri aitumie biashara yake inayorewarewa kuanguaka ili itakapoanguaka kabisa kisa kiwe Dogo Richie.

Sanaa, burudani na Starehe bila kujiekea akiba ni donda sugu linalowaumiza wasanii wengi Kenya. Na leo Amz ameonyesha kweli dunia kwamba, wasanii wameeka starehe mbele zaidi kuliko maendeleo yao binafsi. Kwanini Amz hangeweza kusuluhisha shida zake na Richie nyuma ya pazia? Mbona akaamua kumwaga mtama mbele ya kuku wengi? Ama kachukulia hatua ya Susumila kujibu mapigo ya Muziki majanga ilikutengeneza kiki kama wenzetu wabongo wanavyodai kama nafasi ya kutoa yamoyoni mwake? Basi Amz huenda kachukua hatua ama njia potovu, maana Kenya nzima sasa imeshajua kuwa TEMPOZ studio inachungulia kaburi. Kama mwanabiashara, Amz angetafuta suluhu la kudumu la kuziba pahala panapo vuja, kuliko kutia moto nyasi zote kwa pahala pamoja pavujapo. Kukinyesha ama jua liwakapo basi mwenye nyumba utaabani kwani paa litakuwa limeshauungua, namaliza na msemo huu ''akiba mbii haiozi'' na mgala muue ila haki yake mpe.

Post a Comment

Previous Post Next Post