Richie Ree & Angie| Photo| richie fb

Richie Ree Na Angie

Naanza kwa pongezi kwa wasanii wote hapa Pwani kwa juhudi wanazozipiga ilikuhakikisha wanaipeperusha bendera ya sanaa ya pwani kitaifa na zaidi. Nikisema sanaa, si kimuziki pekee, lakini tasnia nzima ya sanaa mbalimbali ikiwemo, uandishi wa habari, malenga, wanamitindo wa asilia, waigizaji na wanamuziki na nyinginezo. Ila kwa leo nataka kududumiza kipembejo sekta nzima ya muziki wa kizazi kipya Pwani. Na hii inatokana na msukumo wa wimbo mpya wa pamoja kati ya wanamuziki wawili wenye jinsia tofauti, naongelea Dogo Richie na Angie kupitia kibao chao NIPE.

Ujumbe kwenye kibao hiki kwakweli unamakali ya kipekee, napia umeleta taswira tofauti kwenye parawanja ya muziki Africa Mashariki. Kituambacho huwa sirahisi kwani wengi wa wasanii wa muziki wamekuwa wepesi kuiga tungo kutoka kwa wasanii wenziwao ama hata kutohoa santuri pekee (Refix/remix) ila ujumbe ukawa bado niuleule bora tu wachezwe redioni. Lakini msanii Richie Ree kama anavyojiita kwasasa, huwa kabla achilie kibao basi yeye huumiza akili sana kabla ya kuingia studio na kurekodi ngoma. Kwa mara hii Richie akiwa na Angie wamegonga ndipo, kwani ujumbe wenyewe ndio donda ndugu linalokwamisha vipaji vya wasanii wengi wachanga kwenye mchezo huu wa muziki.

Richie Ree Na Amz Producer

Wakinadada wengi wamekuwa na hamu yakutingisha mawimbi ya redio tofauti nchini na hata kimataifa. Licha ya sauti zao nyororo na vipaji lukuki vyenye kuenda shule, wamebaki kutamani kuyafikia malengo yao kwa ndoto za alinacha. Maana ufisadi uliopo kwenye kapu zima la tasnia ya sanaa ya muziki, umepitiliza mipaka na Kibao Nipe kimekuwa ushaihidi wangu wa wazi. Nikipigia muhuri kibao hiki, ulofa na ubebari umewazidi maarifa wasanii wachanga kiasi cha kukata tamaa ya kufikia malengo yao. Kuna msanii mchanga kwa jina Snomey Lee kutoka Kilifi, amekua akilalama kupitia mtandao wa facebook kuwa licha ya kurekodi na kutuma muziki kwa vituo mbalimbali vya redio bado hajaona mafao. Hii nikwasababu amekua aking'ang'ana kujituma usiku na mchana kuhakikisha anatoboa lakini wapi. Siyeye pekee anayepitia hali hii, unapozitembelea studio za kutayarishia muziki hapa Mombasa pekee, utaelewa nini ninacho kizungumuzia. Kwamaana utashuhudia foleni kubwa za vijana wenye kiu na hamu ya kusikika na kuwa nyota nchini kupitia muziki. Lakini kwakuwa wanauhaba wa fedha, basi huishia kwenye mikono ya mabwenyenye wachache wenye kutaka kufaidika kutokana na nguvu zao. Basi hapa ndipo kizungu mkuti kinapotokea, haswa watoto wakike hukiona cha mtema kuni.

Snomey Lee msanii chipukizi kutoka Kilifi

Ufisadi huja kwa njia nyingi, kuna ufisadi wa pesa kwa pesa na ufisadi wa pesa kwa ngono. Urembo wa msanii wa kike huwavutia baadhi ya wasanii wenye nafasi, watayarishi wa muziki na wasimamizi wa wasanii kuwalaghai wasanii wakike kula uroda nao ili wapate nafasi ya kusikika. Hatua ambayo imesababisha tasnia ya muziki Pwani kuwa na wasanii wachache wakike licha yakuwa na wasanii lukuki wazuri ila wapo chini ya maji. Wasanii hawa huogopa sana kutumika kama watumwa kwenye mtanange mzima wa kutengeneza na kusambaza muziki mzuri, kitu ambacho kimeifanya tasnia hii ya muziki wa Pwani kutoimarika na kukuwa zaidi kwani kila uchao wasanii ni walewale. Sijui ni msukumo gani ambao Amz, Richie na Angie wamekua nao hadi kupata hekima ya kuto kibao hiki Nipe. Ambacho kwakweli kinawagusa wadau wengi wa muziki Pwani haswa wale wenye tabia za kuwalaghai wasanii wachanga kwa ulimi wa kuwasaidia kutoboa kumbe wanawapaka mafuta kwa mgongo wa chupa umewvunja mioyo wasanii wengi chipukizi. Naona kibao Nipe kiemwafikia watu wenye hulka kama hii, na ndiposa leo nimeamua kulimulika tatizo hili sugu linalokwamisha muziki wetu wa Pwani.

Post a Comment

Previous Post Next Post