Michael Olunga akiwajibikia klabu yake mpya, Girona FC kwenye mechi dhidi ya hisani dhidi ya  Ripoll FC mnamo Septemba 4, 2017. Olunga alifunga magoli mawili yaliyoiwezesha timu yake kuibuka na ushindi mkubwa wa magoli 8-0
Michael Olunga akiwajibikia klabu yake mpya, Girona FC kwenye mechi dhidi ya hisani dhidi ya  Ripoll FC mnamo Septemba 4, 2017. Olunga alifunga magoli mawili yaliyoiwezesha timu yake kuibuka na ushindi mkubwa wa magoli 8-0

Mshambulizi wa timu ya taifa ya soka Harambee Stars Michael Ogada Olunga alianza vyema maisha yake nchini uhispania alipotinga mabao mawili yaliyoisaidia klabu yake mpya shiriki kwenye ligi kuu Uhispania, Girona FC kuinyuka Ripoll FC magoli 8-0 katika mechi ya hisani iliyopepetwa hapo jana ugani Ripoll kwa ukumbusho wa shambulizi la Barcelona la mnamo Agosti 18 mwa huu.

Girona walitangulia kukiramba kimia dakika ya 10 kupitia kwa Carles Planas, Mnigeria Olarenwaju Kayode aliye kimkopo kutoka Manchester City akafunga la pili dakika ya 27 huku la tatu likiunganishwa na Portu dakika chache ngoma kuingia mapumziko.

Kunako dakika ya 61 kipindi cha pili, Aday Benitez aliipa Girona goli la nne kisha Sajili mpya Olunga aliye kimkopo kutoka klabu ya china ijulikanayo kama Guizhou Zhicheng  akitumia dakika za 71 na 72 kufunga mawili.

Marlos Moreno na Johan Mojica wote kutoka Colombia walifunga goli moja kila mmoja na kutamatisha ushindi huo.

Klabu ya Girona FC inamilikiwa na City Football Group, kampuni inayomiliki pia klabu za Manchester City, New York City, Melbourne City, Yokohama F, Marinos na Atletico Torque ya nchini Uruguay. 


Kakake Pep Guardiola, Pere Guardiola ambaye ni wakala wa mwanasoka Luis Suarez na Andreas Iniesta pia anamiliki asilimia 44 ya hisa za klabu hiyo.


Girona kwa sasa imo kwenye nafasi ya sita katika jedwali la La Liga baada ya kuilaza Malaga na kwenda sare na mabingwa wa ligi hiyo mwaka wa 2004 Atletico Madrid.


Post a Comment

Previous Post Next Post