Gami Dee| Photo By| Gami

Gami Dee| Me Nawe cover

Kutoka Bongo, leo nimukusongezea karibu nawe mkali wa ngoma Twende wote na Kayogo Gami Dee, nyota huyu mwenye makazi yake mkoani Njombe ameamua kuvunja ukimya wake kwa kuachia ngoma yake mpya kwa jina Me Nawe. Gami ambaye pia huwa ni mtandazaji wa kituo cha radio cha Ice FM na pia Television, nikati ya mastaa wachache Africa Mashariki walio jaliwa na vipaji kemukemu ambavyo pia tunajumlisha na kuwa yeye pia ni muandishi mkali mbali na utangazaji na uimbaji. Gami kwa mara nyingi amekuwa mwepesi kukuletea habari tamutamu kupitia blog ama wavuti maarufu Africa Mashariki nchini Tanzania (Bongo Five), na sasa ameamua kuonyesha ama kunoa makali kipaji chake chengine cha uimbaji, na ndio maana kwa wakati huu ameamua kukusogezea utamu kwa kupitia mashairi ya wimbo huu wake mpya nakama nilivyotangulia kusema kuwa jina la wimbo huu ni Me Nawe. Hebu bonyeza kitufe hichi hapa chini kwenye kiunganisho hiki cha utandawazi ili upate kusikia mradi wake mzima hapa chini. Kiambatanisho hiki hapa ni Kwaniaba ya Bongo5 -( Music link is hosted by Bongo 5)Post a Comment

Previous Post Next Post