Kocha wa Ulinzi Stars FC, Benjamin Nyangweso akizungumza na wachezaji wake kwenye hafla ya mazoezi ya asubuhi uwanjani Safaricom Kasarani. Picha/Stafford Ondego/www.sportpicha.com
Kocha wa Ulinzi Stars FC, Benjamin Nyangweso akizungumza na wachezaji wake kwenye hafla ya mazoezi ya asubuhi uwanjani Safaricom Kasarani. Picha/Stafford Ondego/www.sportpicha.com

Klabu ya Ulinzi Stars imetetea ubingwa wake wa Afrika mashariki baina ya vikosi vya ulinzi, makala ya 11 ya mashindano hayo yanayotarajiwa kukamilika hapo kesho jijini Bujumbura, Burundi.


Kwenye mechi iliyopigwa hapo jana adhuhuri katika uga wa Prince Louis Rwagasore, Boniface Onyango alifunga goli la pekee dakika ya 19 lililowanyima wapinzani wao Tanzania ubingwa na hivyo kuibuka wafalme wa mchezo huo wa soka kwa mara nyingine.Kocha mkuu Benjamin Nyangweso amewapongeza wanasoka wake kwa kazi nzuri walioifanya kutetea taji hilo na kusisitiza sasa mawazo ni kweneye ligi kuu KPL.Ningependa kuwashukuru wachezaji wangu kwa kutandaza soka tamu na ya kumezewa mate, hususan mechi hiyo ya fainali dhidi ya Tanzania.Tatizo kubwa nililoliona ni kwa upande wa marefa, wengi wao ni kama hawafuati sheria, wanachukulia tu bila kugaguliwa kama wanaafikia viwango na kuwekwa uwanjani.Baada ya hapa ni kurejea nchini Kenya na kupigania taji la ligi kuu KPL. Naamini kwa jinsi tulivyopata mazoezi ya kutosha kwa mashindano haya ya majeshi, tutajikwamua zaidi katika ligi.


Kwa mashabiki wetu nawaomba waisfe moyo.’” Aliongezea Nyangweso.
Katika ligi kuu Ulinzi imo kwenye nafasi ya nne kwa alama 32 nyuma ya viongozi Gor Mahia, Sofapaka na Posta Rangers.Ulinzi walianza kampeni yao ya ubingwa wa majeshi kwa kuwanyoa wenyeji Burundi bao 1-0 kisha wakaandikisha sare ya 1-1 na Uganda kabla ya fainali ya jumapili.Ushindi wa Ulinzi uliandikisha medali ya nne kwa Kenya kwenye mashindano hayo baada ya kunyakua dhahabu mbili katika vitengo binafsi na mbio za mita 10, 000 kwa wanaume sawa na dhahabu katika mchezo wa voliboli.Tanzania ni ya pili na dhahabu tatu, mbili kutoka mbio za nyika na moja kutoka mchezo wa basketiboli.Ubingwa huo unatamatika hapo kesho huku Kenya ikitarajia kunyanyua ubingwa wa ujumla.
Post a Comment

Previous Post Next Post