Alikiba| Photo by| Kiba fb


Baada ya kutoa kibao chake kikali cha Seduce Me, msanii mkali kutoka Bongo Alikiba amekuwa hashikiki kwa jinsi anavyozizoa show za burudani ndani ya Tanzania. Alikiba ambaye amekuwa miongoni mwa mastaa wa muziki wenye nembo ya (A list) ambao wameshirikishwa kwenye tamasha la Tigo Fiesta 2017, amezidi kuzigusa nyoyo za wapenzi wa muziki Tanzania na nje ya nchi hiyo. Leo nimekusogezea karibu moja kati ya show kubwa kuwahi kushuhudiwa Tanzania ambayo Kiba alitumbuiza umati wa mashabiki wake mukoni Mwanza Tanzania. Tamasha hili la kila mwaka huandaliwa na kampuni ya habari ya Clouds Media wakishirikiana na kampuni ya mawasiliano ya Tigo, na huzunguka mikoa kadhaa nchini Tanzania kwaniaba ya kutuo burudani. Mwaka huu Fiesta ilizuru Arusha, Mwanza na mikoa mingine nchini Tanzania. Kwasasa nimekukonyezea hapa chini burudani lukuki kutoka kwa Alikiba, hebu burudika zaidi kwa kutazama video hii hapa chini.
Post a Comment

Previous Post Next Post