Naibu Rais wa shirikisho la soka nchini Kenya FKF, Doris Petra (kushoto) na Rais Nick Mwendwa wakiongea na waandishi habari mjini Eldoret baada ya mkutano wa wajumbe wa FKF kanda ya kaskazini mwa bonde la ufa. Picha/Kwa hisani
Naibu Rais wa shirikisho la soka nchini Kenya FKF, Doris Petra (kushoto) na Rais Nick Mwendwa wakiongea na waandishi habari mjini Eldoret baada ya mkutano wa wajumbe wa FKF kanda ya kaskazini mwa bonde la ufa. Picha/Kwa hisani
Shirikisho la soka barani Afrika CAF sasa linahofia usalama wa Kenya inapojiandaa kurejelea uchaguzi wa Urais Okotoba 17, huku muda wa kuandaliwa kwa kipute cha CHAN mwakani ukizidi kuyoyoma.

Kwenye mahojiano ya kipekee na Bana Michezo, naibu Rais wa shirikisho la soka nchini FKF, Doris Petra hapo jana alidai hatua ya mahakama ya kilele kubatilisha ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta na kuamua wakenya warudi debeni kutekeleza tena haki yao ya kikatiba, imezua hofu na kulazimu CAF kutuma makamu wake Constant Omari nchini kuchakatua joto la kisiasa.

Tunachohitaji kutoka kwa seirkali ni fedha za kusaidia kuboresha miundo mbinu.

Tunaye waziri na wasaidizi wake wanaowakilisha serikali kwa hivyo endapo hela zilizoidhinishwa zitatolewa kwa wakati basi hilo huenda likatimia vyema.

Ningependa kuwaambia Wakenya wote kwa ujumla wombe na kuhubiri Amani na kuwa Chan itaandaliwa nchini sawa na taji la mataifa bingwa Afrika mashariki, Cecafa kabla ya mwaka kuisha.

Huku ukarabati wa nyuga tano zilizotengewa uandalizi wa kipute hicho ukishika kasi, Petra yu na imani kuwa uchaguzi huo hautaathiri mchakato mzima huo.

Makamu wa Rais wa CAF tayari yumo nchini baada ya kuwasili Jumapili na kupokelewa na mwenzake ambaye Rais wa FKF, Nick Mwendwa.

Walifanya kikao na serikali kutathmini suala la usalama kutokana na kurejelewa kwa uchaguzi wa Urais na kwangu mimi nadhami amani itadumishwa jambo litakalotufanya kuandaa CHAN.

Afisa mkuu mtendaji wa FKF Robert Muthomi kwa upande wake ameungana na Petra kuamini kuwa CAF itaridhishwa na maandalizi ya CHAN nchini.

Nataka kusema kuwa shughuli ya ukarabati wa viwanja inaendelea vyema ila uamuzi wa mahakama ya upeo Ijumaa iliyopita, umefanya CAF kutilia hofu suala la usalama.

Kutokana na hilo, Caf imemtuma makamu wake wa Rais nchini kujadiliana na serikali pamoja na shirikisho la FKF kuhusu suala ya usalama na natumai wadau husika watapeana maelezo mwafaka yatakayohakikisha kipute cha CHAN hakipelekwi nje ya taifa hili la Kenya.

Post a Comment

Previous Post Next Post