Umar Kasumba wa Sofapaka akichupa juu angani kuunganisha goli dhidi ya kipa wa Muhoroni  Youth  Sowedi Salim  kwenye mechi ya ligi kuu KPL baina ya pande hizo mbili ya mnamo jumamosi ya Julai 29, 2017 ugani Nyayo. Kasumba. Picha/soka.co.ke
Umar Kasumba wa Sofapaka akichupa juu angani kuunganisha goli dhidi ya kipa wa Muhoroni  Youth  Sowedi Salim  kwenye mechi ya ligi kuu KPL baina ya pande hizo mbili ya mnamo jumamosi ya Julai 29, 2017 ugani Nyayo. Kasumba. Picha/soka.co.ke

Mabingwa wa mwaka wa 2009 wa ligi kuu Kenya KPL Sofapaka wametwaa taji la mwanasoka bora wa mwezi kupitia kwa wachezaji wao wawili wote raia wa Uganda, nazungumzia Umaru Kasumba na Rodgers Aloro waliotajwa wote wachezaji bora wa mwezi Agosti na ikiwa ni mara yao ya kwanza.Wawili hao walitoa mchango mkubwa kwa vijana hao maarufu Batoto Ba Mungu timu hiyo ilipocheza mechi tano bila kufungwa kwenye ligi ya KPL na kuifanya kuinuka kutoka nafasi ya tano hadi ya pili kwenye jedwali baada ya ushindi mara nne na sare.Kutokana na kutambuliwa kwao, waganda hao waligawana shilingi 30,000 fedha za Kenya zinazotuzwa mwanasoka bora wa mwezi, kumaanisha kila mtu aliondoka na shilingi elfu 15 ila Kasumba akatabasamu zaidi baada ya kuongezewa hela zingine shilingi elfu 30 kwa kuibuka mfungaji bora wa mwezi Agosti,akichana mabao sita kufikia sasa katika kampeni ya ligi.Mganda huyo alifungua akaunti ya mabao kwenye mechi dhidi ya Muhoroni Youth waliyoshinda kwa mabao 3-1 kisha akasonga mbele na kufunga kwenye ushindi wa 3-0 dhidi ya Thika United, sawa na ushindi wa 5 – 2  dhidi ya Nakumatt FC, alafu akapiga mawili katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Nzoia  kabla ya kufunga mwezi na kufunga bao la kusawazisha kweneye sare ya 11 na Posta Rangers.Kumpata mshindi, kamati ya kiufundi ilipigia mwanasoka bora kura kwa kila mchezo kwa mwezi huo na mwisho wa siku mchezaji anayependelewa kwa sana hupokea tuzo.Kwenye mechi dhidi ya Muhoroni Youth, Feni Ali  alitajwa mchezaji bora, Aloro ambaye ni beki akatajwa mara mbili mfululizo kwenye ngoma dhidi ya Tusker na Nkaumatt ambapo alifunga mabao matatu katika kila mechi hizo kisha Kasumba akatajwa mchezaji bora kwenye mechi ya Nozia.


Post a Comment

Previous Post Next Post