Stevenson| Photo By| Changez Ndzai


Muziki ni mwito, na mwito huu unapokolea huwaka moto. Ila kama ujuavyo moto hauwaki mpaka dalilize kujitokeza, ambazo moja wapo niuwepo wa kufuka kwa moshi hewani. Tanzania ni nchi ilio jaa vipaji, pia kimuziki Africa Mashariki na eneo zima la maziwa makuu nchi hii inaongoza na hili halina ubishi. Wasanii ambao wanao sifika huwa kunamahali wanaanzia, hivyo siwote wanao chipuka na kufika juu kwa ghafla hapana. Ila kukua kimuziki huwa ni hatua baada ya hatua. Hapa ndipo ninapokuja na maada nzima ya makala haya ya leo.

Stevenson| Photo By| Changez Ndzai

Msanii Stevenson Katika Ubora Wake

Stevenson ama ukipenada mwite Steve Tanzania, nikati ya wasanii wanao fanya vyema kwenye game ya muziki Tanzania na pia upande wapili wa tasnia ya filamu maarufu kama Bongo Movie. Steve pia anahulka ya ulimbwende ndani yake, kwa jinsi anavyo jibeba kimavazi na muondoko wake wakuhakikisha anawavutia mashabiki wake kwa utanashati wake. Kama vile wasanii wengine, amekua mwepesi wa kusoma kutokana na makosa ya wasanii wengi ilikuhakikisha kua hayarudii makosa hayo. Tayari ameanza michakato ya kupambana na soko la muziki Africa Mashariki licha ya changamoto zilizopo kwenye game hii. Kwasasa ameanza kujinadi, na kujifunga kibwebwe ilikuhakikisha muziki wake unavuka boda na kupenya nchini Kenya huku akiwa na kibao kipya kibindoni kwajina Natamani. Kama kawaida yetu hapa EaBana, kupitia meza yetu ya Celeb Crush tumekitambua kipaji cha msanii huyu nakama walivyosema wahenga, chanda chema huvishwa pete TAYARI tumemuvisha.

Post a Comment

Previous Post Next Post