Nyashinski Mteule Kwenye MTVEM AWARDS 2017


Jina la Nyashinski limegeuka kuwa alimasi, hii nibaada ya kutokea kwenye orodha ya mastaa wa Africa waliorodhoshwa kwenye msimu mpya wa mwaka huu 2017 wa MTVEMA. Hii ni kwasababu nyota huyu wa hapa nchini Kenya, amekua akitoa hit baada ya hit tokea aliporudi kutoka ughaibuni alikoenda kudumu kwa kiasi cha muongo mmoja. Kitengo hiki alichoteuliwa ambacho mwaka wa 2014 kilitwaliwa na na kundi la muziki barani Africa Sauti Sol kutoka hapa nchini Kenya, pia kimeshawahi kuwakilishwa na majirani zetu Watanzania nikizungumuzia Diamond Platnumz na Alikiba ambaye ndiye aliyenyakua tunzo hiyo mwaka jana 2016.

Hata hivyo ndugu zetu Watanzania hawajafurhishwa na hatua yakuwa mastaa wao hawajatokea kwenye orodha hii ya tunzo za MTVEMA 2017. Hatua ambayo imezua mjadala na mgogoro kwa makundi mawili hasimu ya muziki nchini Tanzania maarufu kama team Kiba na team Mond. Huku kila upande ukilaumu upande mwingine kwa kuchangia staa wanayependa kutotajwa kwenye tuzo hizi maarufu na zenye hadhi kubwa duniani. Hata hivyo Mastaa mbalimbali nchini Kenya wamekuwa wepesi wakuonyesha furaha yao didhi ya uteuzi wa Nyashinski, huku Sauti Sol wakiwa kwenye mstari wa mbele kumpigia debe Staa huyu wa Kenya ili kuwabwaga wapizani wake wakiwemo Davido na Wizikid wote wa nchini Nigeria. Hapa chini ni baadhi ya screen-shot za comments za Watanzania mitandaoni, baadaya tavuti maarufu ya Millard Ayo kupost habari hizi kwenye ukurasa wake wa Facebook. Hebu cheki majirani zetu ndani ya Bongo walivyotoana povu siku nzima ya leo sababu niuteuzi wa Nyashinski kuiwakilisha Africa Mashariki.Post a Comment

Previous Post Next Post