Kikosi cha Kenya Simba kwenye mechi ya awali. Picha/Kwa hisani
Kikosi cha Kenya Simba kwenye mechi ya awali. Picha/Kwa hisaniTimu ya taifa ya mchezo wa raga kwa washirki 15 kila upande kwa wanaume maarufu Kenya Simba imeangukiwa na pigo ikielekea kwa mechi yao Jumamosi hii dhidi ya wenyeji Hong Kong kwenye taji linaloshirikisha mataifa manne, hii ni baada ya mchezaji wao mahiri wa kiungo cha mbele Joshua ‘Reign’ Chisanga kuripotiwa kuwa huenda akakosa pambano hilo.

Chisanga alichechemea kwa maumivu kwenye kichapo cha Jumamosi iliyopita cha alama 10-31 mikononi mwa Urusi, katika uga wa Kings Park Sports nchini Hong Kong. Muungano wa mchezo wa raga nchini KRU hii leo umethibitisha kuwa mchezaji huyo hatashiriki kwenye mechi hiyo .

Wakati uo huo takwimu za Simba zimeporomoka kutoka nafasi ya 27 hadi ya 29 baada ya vichapo viwili mtawalia huko Hong Kong.


Post a Comment

Previous Post Next Post