Snomey Lee Msanii Chipukizi| Picha Na| Changez Ndzai

Snomey Lee Msanii Chipukizi Kutoka Kilifi Kaunti


Katika hali halisia yakuhakikisha vipaji vya wasanii vinatambulika, basi EaBana huwa inabidi kuzama chini kabisa tofauti na wengine. Muhimu kabisa nikuhakikisha kuwa tunagundua, chimbua na kusukuma talanta ambazo zipo lakini watu wanazidharau na kuzipuzia. Wengi kwasasa  tu wanafahamu hali ngumu aliyopitia msanii Diamond Platnumz kabla ya kuupata umaarufu. Pengine hata wengi hawajui kabla ya kuanza kuimba Diamond alikua Rappa. Na japo alikua akijimudu ili kuhakikisha anapambana vilivyo kwenye game, staa huyu alikumbwa na msongo ama changamoto nyingi katika safari yake ya muziki. Hata baada ya kupata fursa yake ya kwanza yakuanza kusikika chini ya mikono ya mtaarishi wa muziki na msanii mwenza wa muziki wa Bongo Flava Bob Junior, zilizuka changamoto mpya ambazo ziliwafanya kukosana na mtayarishi huyu wa muziki na kutafuta studio nyingine mbali naile ya Bob Junior.

Diamond Platnumz| Photo Courtesy| Diamond Facebook

Diamond Platnumz Hatua hii ndio inanisukuma mimi binafsi kuwatafuta wasanii wachanga wanao kuwa na ndoto yakuwa mastaa ila licha ya kurekodi muziki nakuutuma kwa radio mbalimbali basi wamekua wakichamba makopa. Katika kauti ya Kilifi, kuna wasanii wengi kama hawa ambao wanajaribu kutambulika ila nafasi hii imekua adimu kwao. Snomey Lee nikati ya mfano wa mastaa hawa, licha yakujituma nakutaka jamii kutambua kipaji chake kama msanii, hatma ya ndoto yake imemuwia ugumu hadi kuamua kutumia mtando wakijamii kuanika uchungu wake. Kitu kilichonifanya kumsaka nakutaka kujua nini haswa kinachomsukuma kuueleza uchungu wake didhi ya kukosa msukumo kutoka kwa vituo vya redio Pwani licha ya kujituma. Je waendeshaji vipindi vya burudani redioni hapa Pwani ndio wakulaumiwa ama wanamuziki ndio wenye balaa?

Ni njia gani msanii mchanga anafaa kuipitia ili kuhakikisha kua anafanikiwa kufikisha muziki wake redioni na kuchezwa? Swali hili nigumu, kwamaana kwa upande mwingine nimekuwa nikijadiliana na watangazaji wa vipindi vya burudani na si Pwani ya Kenya pekee bali hadi Tanzania. Na basi kwa upande wa watangazaji wamekuwa wakilalama kuwa wasanii wachanga huwa wanataka makubwa wasiyoyafikia kwa haraka. Hutaka kujilinganisha na mastaa wakubwa nakushindana nao kabla hata ya hao kutambulika. Hujenga kiburi na kubadilika licha tu ya nyimbo zao kuchezwa mara mbili ama tatu kwa redio tofauti. Hali ambayo inawaumiza watangazaji, na imepelekea watangazaji wengi kuganda kujiingiza katika hali kama hii kwa kuwa makini kupeana musukumo kwa wasanii watakao wasaliti punde tu mlango wa ufanisi unapo jitokeza. Wengi wa wasinii wachanga humea nundu na hujenga jeuri na kiburi na wanapo jaribu kurekebishwa basi huwa wepesi wa kurusha cheche za matusi kupitia mitandao ya kijamii.

Ushauri wangu kwa wasanii kama Snomey Lee, msanii chipukizi anafaa awe na nidhamu. Hekima na uvumilivu kwani muziki kama biashara zingine unachangamoto zake. Acha nipeane mfano muzuri ni kampuni ya Mawasiliano ya Safaricom. Hii nikati ya Kampuni zilizo na mafanikio makubwa barani Africa. Lakini pengine watu wengi wamekuwa wakiona ufanisi wao pekee ila pia hao wako na changamoto wanazokumbana nazo kila siku. Moja wapo ikiwemo ile inayoshuhudiwa kwasasa, ya baadhi ya wateja wake kujiondoa kutoka kwa kampuni hii na kujiunga na kampuni pinzani kwa msimo wa binafsi. Je unajua nikwakiasi gani kampuni hii inatumia nguvu kukabiliana na tatizo hili? Hivyo ndinyo ilivyo kwa kila bishara.

Hivyo nidhamu, uvumilivu na heshima nivigezo mhimu kwa msanii yeyote hata wale walio fanikiwa. Lazima msanii ajinyenyekeze na kukubali kufata njia atakazo elekezwa na wadau wa muziki ili kufanikiwa. Kila mja anabaraka zake, maana hata walumbi walishanena tokea zamani kuwa bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi. Hivyo usivae viatu vya msanii mwingine aliyejuu yako nakutaka kupitia njia kama zake. Jaribu kuwa mpole na kutafuta njia mbaadala zakukuletea mafanikio. Watayarishi wa vipindi, watangazaji wa habari na wadau mbalimbali kwenye kiwanda cha burudani haswa muziki, ni binadamu pia. Japo wanauwezo tofauti na wako pia huwa na hisia. Kwahivyo unapoakuwa unataka msaada kutoka kwao, jaribu kuitimia akili na usiwemwepesi wa kulalama ila vumilia na kupigania kushinda halingumu kwa njia tofauti usije ukawakwaza nakupelekea kujitenga mbali nawe. Na lamwisho kabisa usisahu kumuomba Mwenyezi Mungu na kumueka mbele kwa kila kitu unachokifanya na utacheka.

Post a Comment

Previous Post Next Post