cHANGEZ NDZAI| PHOTO| CHANGEZ

Wakati siasa za nchini Kenya zinavyozidi kupamba moto, sanaa ya nchini Kenya pia imekuwa ikipata pigo kwa jinsi mambo yalivyo magumu haswa kwa wasanii. Lakini hata hivyo, kitu ambacho kimezua hisia tufauti kabisa na kuchochea moto wa kisiasa kuwaka hata zaidi ni hatua ya viongozi wa kanda ya Pwani ya Kenya wakiongozwa na gavana wa Mombasa Hassan Joho na mwenzake wa Kilifi Amason Kingi yakutaka kujitenga mbali na Kenya. Hatua ambayo imeonekana kuungwa mkono kwa asilimia tisaini na nane (98%) na wakazi wa Pwani wanaodai kuwa wamekuwa wakidhulumiwa na kuhujumiwa kwa miaka mingi toka Kenya kujinyakulia Uhuru mnamo mwaka wa 1963.

Sitaki kuingilia sana siasa, kwasababu nia yangu nikuhakikisha nalibingirisha gurudumu la burudani kwenda juu zaidi. Nikilenga sana sanaa mbalimbali na wasanii kutoka sehemu zote za dunia. Ila kwakuwa mimi chimbuko langu ni Pwani ya Kenya, naona jambo hili linanihusu ingizingatiwa kuwa mimi pia ni mmoja kati ya wasanii wanaoiwakilisha Pwani ya Kenya Duniani kupitia uandishi, kuripoti habari za matukio ya burudani kwa redio Afrika Mashariki na Umalenga. Mfumo wa uongozi wa kauti unaotambulika kikatiba nchini Kenya, ambao ndio unaotumika kwasasa uko kwenye majaribio. Nasema hivi kwakuwa, kwasasa tangu uidhinishwe naakuanza kufanya kazi rasmi mpka sasa unaumri wa miaka mitano tu. Nakatika miaka hii mitano, asilimia kubwa ya wasanii wa Pwani wamekua wakilalama kutopata misaada na ushirikiano mzuri kutoka kwa serikali za kauti.

Changez Ndzai| Photo by| Changez Ndzai

Magava Wa Pwani Kuanzia Kushoto Jeffa Kingi Na Ali Joho Katikati Wakati Wa Mkutano Uliopita.

Hili kweli sijambo la kuzua mjadala, kwani ni wazi kabisa kuwa serekali za kauti za Pwani ya Kenya zimekua vipofu kwa swala lakuwekeza kwenye kiwanda cha burudani na sanaa mbali na michezo. Kauti ya Mombasa japo kupitia Gavana Joho imekuwa na mikakati ya kuhakikisha wasanii wa kauti hii tajika wanapata fursa ya kuwasilisha vipaji vyao kupitia matamasha kama vile Tukutane Mombasa ila hatahivyo, anahitajika kufanya zaidi ya hivyo maana pia  yeye Gavana Joho amekuwa akituhumiwa na wasanii wengi wa kauti hiyo kuwa amekuwa mwepesi wa kusukuma kazi za wasanii wa nje ya Kenya mfano Tanzania zaidi kuliko wale wasanii wake ambao pia niwapigaji kura. Je kutokana na taswira hii, wasanii wanatamaa yakuwa watafanikiwa kimaisha kupitia sanaa kama Pwani ikijitenga kotoka Kenya nakuwa nchi binafsi? Mimi binfsi naona kunauwezekano wa viongozi wa Pwani kubuni fursa na nafasi zaidi za kazi kupitia sanaa iwapo mbiu muundo msingi zitazingatiwa.

Changez| Photo by| Changez Ndzai

Kutoka Kushoto Gavana Joho Akicheza Pamoja Na Msanii Alikiba Toka Tanzania Kwenye Tamasha LililopitaNikitupia mfano wa Zanzibar ama Zanziabari, ambako pia nafanyia kazi kituo cha redio cha Swahiba FM 102.9 kama ripota wa habari za burudani. Ninasoma mengi kupitia Kisiwa hiki kwaani wasaanii wa Zenji aka Zanzibar wamekuwa wakitamba bila woga nakuongoza chati za muziki Afrika Mashariki, sababu ya musukumo wanaopewa na serikali ya kisiwa hiki japo pia wapo chini ya serikali kuu ya Muungano wa Tanzania. Wasanii wa Zenji akiwemo marehemu Bi. Kidude (Mungu ailaze rohoye pema peponi) na kundi maarufu la muziki la Offside Trick japo kwasasa limesambaratika, ila kupitia mfumo wa matangazo na musukumo wa muziki Zanzibar wasanii hawa walitambulika na bado wanatambulika kwa mchango wao kisanaa. Matamasha makubwa ya kusukuma sanaa kama vile Zanzibar Music Festival, yamekuwa yakitumika kuusukuma na kuutangaza muziki na wanamuziki wa Zanzibari kwa kiasi kikubwa huku ikivutia wasanii wakubwa si Tanzania bara pekee ila hata mashabiki kutoka kote dunia huja kufurahia utamu wa sanaa na kushuhudia vipaji vya wasanii kemukemu kotoka zanziabar hivyo basi kufungua nafasi za biashara na kazi kwa watu mbalimbali wakiwemo wasanii wenyewe.Video: Jinsi Tamasha la Sauti Za Busara Za Zanzibar Lilivyonoga  Mapema Mwaka Huu 2017.


Je kama viongozi wetu hapa Pwani wameanza mchakato wakujitoa kutoka nchi ya Kenya nakuwa nchi inayojitegemea kivyake, wataweza kweli kuiboresha sanaa ya Pwani na kuwa kiwanda cha kivyake nakubuni nafasi za kazi kwa wasanii? Ama wanafikiria tu hoja zao binafsi tu? Nafikiria makala haya yatawafikia wadau husika katika ofisi za kauti zote za Pwani ikiwemo Kauti ya Mombasa, Kilifi, Kwale na Lamu. Utangamano, uwazi na kwikwi za kupinga ubinafsi zinaweza kuwa njia mbadala yakuwasaidia zaidi wasanii wa Pwani ambao kwasasa wako katika hali hobelahobela kwani kusema kweli hawajivunii bidii ya jasho lao wanalolitoa kwa kurekodi na kuuza muziki. Ingawa vituo vya habari vimekuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wanawapa sapoti wasanii hawa. Kunauwezakanao kiwango cha kipato kinachotokana na utozaji ushuru katika kauti za Pwani kikachangiwa pakubwa na mchango wa sanaa. Ila yote inawezekana kama viongozi wetu wataweza kuwajenga wasanii kwa kuwapa fursa ya kutalii kazi yao ya sanaa mithili ya Watanzania wanavyo enzi na kujivunia talanta za wasanii wao. Kama hivi ndivyo nchi tarajiwa ya Pwani itaweza kufanya, basi hata mimi nitaiunga mkono, ila kama hali itabakia ile ile tuliyoishuhudia miaka mitatno iliyopita basi heri wazo hili la kujitenga kutoka Kenya na kuwa nchi huru libaki kuwa ndoto.

Post a Comment

Previous Post Next Post