Aliyekuwa mkufunzi wa Ivory Coast Marc Wilmots. Picha/Getty Images
Aliyekuwa mkufunzi wa Ivory Coast Marc Wilmots. Picha/Getty ImagesKocha wa ubelgiji Marc Wilmots ameacha kazi ya kuifunza timu ya taifa ya Ivory Coast hii leo, hii ni baada ya kushindwa kuisaidia taifa hilo la Afrika magharibi kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao nchini Urusi.


Ivory Coast ilipoteza nafasi yao ya kucheza kwenye kombe hilo la dunia kwa kusagwa mabao 2-0 na Morocco Jumamosi iliyopita, hatua iliyolazimisha mazungumzo baina yake na shirikisho la soka nchini humo.


Wilmots mwenye miaka 48 aliyewahi kuifunza Ubelgiji alikuwa ametia siani kandarasi ya miaka miwili na cote d' ivore  mnamo mwezi Machi iliyokuwa na uwezo wa kurefushwa kwa miaka miwili zaidi.Post a Comment

Previous Post Next Post