Wachezaji wa Kenya wakipasha misuli moto uwanjani Kenyatta Machakos baada ya kuvuna ushindi kwenye mechi dhidi ya Uhabeshi. Picha/SportPicha
Wachezaji wa Kenya wakipasha misuli moto uwanjani Kenyatta Machakos baada ya kuvuna ushindi kwenye mechi dhidi ya Uhabeshi. Picha/SportPicha

Timu ya taifa ya soka kwa akina dada chini ya miaka 20 haina wasi wasi wowote inapojinga kushiriki mechi ya duru ya pili, kufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya Ghana.


Chipukizi hao wa  Harambee Starlets walinyukwa mabao 5-0 katika mkondo wa kwanza ugenini mnamo Novemba tarehe 5 na hivyo watategemea kipindua kipigo hicho pande hizo mbili zitakaporejeleana Novemba 19.


Licha ya wadau wengi kukosa imani na vipusa hao, kocha mkuu Caroline Ajowi hajakata tamaa na anashikilia kwamba watajituma kuwafunga wapinzani hao kwenye mechi hiyo itakayosakatwa ugani Kenyatta, Machakos.
“ Nadhani tulicheza mchezo wa kujihami katika duru ya kwanza ila kwa sasa tutazingatia sana mashambulizi. Ni sharti tushinde mtinange huo kwa kuwa tunahitaji magoli zaidi,” alisaili Ajowi.
Timu hiyo baada ya kurejea nchini wiki jana kutoka Ghana, ipo katika kambi ya mazoezi uwanjani Kenyatta mjini Machakos kujipanga kwa gange hiyo ya duru ya pili na kwa mujibu wa kocha Ajowi, warembo wana mshawasha mkubwa sana wa kutamba.“Naweza kusema warembo wanajiamini sana na wanatia bidii ili kunakili matokeo ya kuridhisha. Alisema Ajowi aliyeongezea kuwa. “Katika mchezo wa soka chochote chaweza fanyika.”Jumla ya wachezaji 24 wamo kambini huku nyuso geni zikiwa za Sharon Zainab kutoka shule ya upili ya wasichana ya Nginda na Sarah Muthoni wa  Kariobangi North Girls.


Post a Comment

Previous Post Next Post