Ado Biggy
 
Katika pita pita zetu mtaani, kalamu yetu ya EaB ilifika hadi mjini malindi nakukutana na nyota wa mziki anae ibuka kwa jina Ado Biggy. Hebu tumpe sikio ili tuweze kusikia nini alichonacho kwasasa kuhusu mziki wake.


EaB: Ado Biggy ninani?

Ado B: Ado Biggy nikijana mtanashati kutoka Malindi.

EaB: Ado ni jina lako halisia ama jina la sanaa?

Ado B: Jina lamgu la serikali ama halisia mimi naitwa Ahmed Ali Abdalla, ila kwa sanaa ndio najiata Ado Biggy ama unaeza niata Nyati de Rude Boy.

EaB: Ulianza lini mziki?

Ado B: Nilianza mziki nikiwa bado katika shule ya msingi, na nilikuwa nikishiriki kwenye matamasha ya sanaa na michezo huku nilibobea sana upande wa kukariri mashairi.

EaB: Umeataja mashairi, wewe ni malenga?Ado Biggy aki enjoy maadhari ufukweni.


Ado B: Yap, naeza sema mimi ni malenga, sababu hutunga mashairi ndio niimbe kama nyimbo. Yani kwa ufupi napenda mashairi na mistari ya freestyle tangu nikiwa mdogo kama darasa la tano.

EaB: Sasa nieleze, ulianza mziki rasmi lini?

Ado B: Nilianza mziki rasmi mwaka wa 2015, wakati huo nikiwa nchini Qatar. Nilirekodi vibao viwili nikiwa huko halafu nikaendelea pole pole.

EaB: Sikuhizi wanamuziki wengi wako na uongozi, vipi wewe je uko na uongozi?

Ado B: Kwasasa mimi sina uongozi wala studio maalumu ya kurekodia mziki. Ila nimeshikilia studio moja kwa jina solid records na producer Mitaa Kisauni.

EaB: Uko na maneno gani ya mwisho, kuwambia mashabiki wako?

Ado B: Niko na ndoto kubwa katika mziki, maana namini Mungu hakunipa hiki kipaji bure. Japo kuna changamoto nyingi lakini naamini Mungu anasaidia.

Post a Comment

Previous Post Next Post