Diamond Platnumz

Msanii Diamond Platnumz ni mfano wa kuigwa si hapa Africa Mashariki pekee, bali bara Zima la Africa. Wakati anapojivunia kupata mafanikio makubwa kupitia tasinia ya muziki, sikitu cha kubeza ila ni kwa niaba ya furaha anayoipata kila mja wakati wowote ule anapofikia malengo fulani kimaisha. Japo wengi hawajakubali hivyo, kuwa Diamond ni nyota inayoong'aa ama wanafahamu hilo ila wanaogopa ukweli uliowazi kuwa jamaa huyu kwasasa hashikiki, kwani hatua zake zakutaka kuipeleka nchi yake mbele kupitia muziki hazina wa kulinganisha.

Ila kama mwenyewe alivyotangulia kuimba na kusema ''Mie mti wenye matunda milele siachi kupigwa mawe'' Diamond kwasasa anakabiliwa na matatizo yakutengenezwa na Watanzania wenzake. Watanzania walewale walio mpigania kumpandisha juu, leo hii wameaanza kuweka mikakati na vikwazo vyakumteremsha chini Mwana, ndugu na rafiki yao wenyewe. Si ajabu hata vile visa mrembo Hamisa Mobeto amekuwa akifanya hadi kumfikisha mahakamani nguli huyu wa muziki ikawa moja ya mbinu ambayo maadui wake wameitumia ili kuhakikisha jemedari huyu wamuziki anaporomoka na kufilisika kabisa.Tayari kuna taarifa yakuwa kuna vyombo vya habari vinne vikuu nchini humo ambavyo kwasasa havichezi muziki wa kampuni nzima ya WCB. Yaani namaanisha vyombo hivi vya habari havichezi si muziki wa Diamond Platnumz pekee ila wasanii wote walio chini ya Diamond Platnumz akiwemo Rich Mavoko, Rayvanny Boy, Konde Boy a.k.a Harmonize, Lavalava na Queen Darling. Hii niishara ya kuwa Diamond amekuwa tishio kubwa hata kwa vyombo vya habari nchini mwake huku asilimia kubwa ya chanzo cha kupata musukosuko huu ni kwasababu ya kuanzisha vituo vya habari vyake mwenye ikiwemo Wasafi TV na Radio.


 
Diamond akiongelea kuhusu media zinazo mbania
 
Akiongea na vyombo vya habari hivi majuzi jijini Dar es Salaam, Diamond alisema hatishiki wala hatorudi nyuma na msimamo wake wakuipeleka Tanzania mbele kupitia juhudi zake kimuziki na kibiashara. Diamond anasema kufungua milango ya kibiashara kupitia media house Tanzania sikwakujionyesha ila tu nikwasababu anataka kufungua milango ya ajira kwa vijana wenzake. Diamond anakuwa msanii wa pili nchini Tanzania kufungua kituo cha habari chake binafsi baada ya AY japo Diamond ameenda mbele zaidi na kuboresha wazo la AY lakuwa na kituo cha habari bora zaidi na cha kisasa. Hali inayowapa mhaho wamiliki wa vyombo vya habari wengine nchini Tanzania.


Nembo ya Wasafi TV


Hata hivyo vita hivi didhi ya Diamond havija muacha nyota huyu pazuri, kwani tayari athari za musukumo wa mawimbi yameanza kumtoa mapovu mwanamuziki huyu, hali inayompelekea kupunguza mwili kwa ghafla kitu ambacho kilipelekea menejimenti yake kutoa taarifa kwa vyombo vya habari na kueleza kwanini staa huyu kampuza mwili kwa ghafla. Huku ikizingatiwa kuwa ni kawaida kwa Watanzania kutumia mbinu kuwa angusha mastaa wao pindi tu wanapofikia viwango vya juu kupitiliza kimuzi. Tayari Lady Jay Dee alishafikiwa na rungu hili, wako wapi waki na Q-Chilla, Mb Dogyy Mana, Khasim Mganga, Z Antony, Matonya na wengine wengi. Japo Diamond anapambana acha tuone kama kweli ataweza kuwakabili Watanzania wenzake wanao mpiga vita siku baada ya nyingine.

 
 TID akilalama jinsi cartels za muziki zinavyouwa wasanii Tanzania kupitia Wasafi TV.

Post a Comment

Previous Post Next Post