Wasanii Richie Ree na Lava Lava


Msanii wa muziki wa Bongo flava na anayetokea kwenye label kubwa ya muziki iliyoko na makao makuu nchini Tanzania maarufu kama WCB ambayo pia inaongozwa na superstar Diamond Platnumz kwa jina Lavalava, jana aliachia kibao kipya kikiwa tayari kimeandamana na video yake kwa mpigo kwa jina Go gaga. Ikizingatiwa tayari, msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka hapa Kenya maarufu kama Dogo Richie alikua ametangulia tayari kuachia kibao kwa jina lilo hilo Go gaga akiwa amemshirikisha rapper anayechipuka kwajina la Kabagazi ndani ya mieezi mitatu iliyopita na video ya kibao hiki ikapaishwa kwenye channnel ya YouTube. 


Mjadala umezuka nchini Tanzania, huku wengi wa wafuasi wa Lava Lava wakishangaa kama yeye ndie aliyemuiga msanii Dogo Richie ama Richie Ree ndie aliyeiba idea ya wimbo huu. Kitu ambacho kinazidi kutia kizunguzungu ni kwamba, kibao hiki hakikurekodiwa kwenye studio za WCB kama ilivyokawaida ya wasanii wote wafanyavyo ambao wapo kwenye label hii ya WCB. Swala hili limeleta tumbo joto ndani ya Tanzania kwasasa, huku wengi wa kizua shauku kuwa WCB vile ni label kubwa huenda ilinunua idea ya wimbo huu wa Go gaga kwa msanii Richie Ree kutoka  Kenya. 

Wasanii Richie Ree na Kabagazi

Hata hivyo kunao mashabaki ambao wanaamini kuwa, Lava Lava ndie muanzilishi wa idea hii ya Go gaga na muziki huu aliufanya miaka ya awali kabla ya kuingia WCB na baada ya kushauriana na meneja wake Ricardo Momo, basi wakaamua kuitendea haki na kutengeneza video akiwa kwasasa yupo chini ya label ya muziki ya WCB. Hatua hii imepigiwa muhuri na C.E.O wake Diamond Platnumz, ambaye jana kupitia akaunti yake ya Instagram aliipandisha na kualika mashabiki wao wa W.C.B kuipa msukumo kwa kuitazama kwa wingi kwenye YouTube channel yao. Je Dogo Richie anayapi ya kusema kulingana na swala hili? Hatua za kumsaka Richie Ree zipo sambamba na pindi nikimpata basi ukweli wote utabainika hapa. Ila chamsingi ni, inaonekana msanii Dogo Richie anaushawishi flani kwenye ulingo wa muziki ndani ya nchi ya Tanzania. Hebu tazama video  ya Go gaga ya Lava Lava hapa chini.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post