Aisha Mwajumla akiwa kwenye pozi lake.

Aisha Mwajumla, alianza kuigiza akiwa na miaka 6 akiwa chekechea. Ni mtoto wa mwisho katika Familia ya watoto watatu, Alisomea shule ya upili ya Waa girls aliigiza kwenye drama festivals na alipofika kidato cha tatu alijiunga na Likoni sec ambako hakukua na drama club na kuwa miongoni mwa wale walioanzisha club hiyo. ''Nilipokua chuo kikuu (TUM) pia nilikua kwa drama club na Music club. Nimefanya stage plays kadhaa na movie moja, na PETE ndio Tamthilia yangu ya kwanza.''

Aisha anabidii ya mchwa na kutokana na moyo wake uliojaa uvumilivu ameweza kufikia malengo yake japo mwenyewe nasema ndio kama mkoko unaalika maua. Chambilecho wahenga mtaka cha mvunguni sharti ainame. Basi bidii hii aliyoianza tangia Chekechea, Shule ya upili, chuo kikuu hadi sasa, ndio imefikisha hapa alipo leo. Akiwa pia aliigiza kwenye filamu ya Watatu iliyochezwa na SAFE PWANI na kwasa Pete ndio tamthilia yake ya kwanza kuigiza na anaigiza kama NIMIMI, mkewe MBURA. Usisahau kua malkia huyu wa filamu hakupitia chuoni kutazama nyenzo wanagenzi wenza, ila kwa kudra za Mwenyezi Mungu aliweza kutamba kimasomaso kwani  chuoni kikuu humo TUM aliweza kufaulu kusomea Taaluma ya uandishi wa habari. Kupitia wino wangu kama mwandishi kwenye jarida hili la East Africa Bana, tumeona ni bora kukusongezea mrembo huyu ili upate kumfahamu nyota yake  ambayo si Africa Mashariki tu inaitazama bali Africa kwa ujumla inatazamia makuu kutoka kwake.


Makala: Yamehakikishwa na Yusuf Dalu, kuhaririwa na kunakilawa na Changez Ndzai

Post a Comment

Previous Post Next Post