Ni kati ya mastaa wanao ng'ara kwa kina katika ulingo wa sanaa ya uigizaji Africa mashariki. Alianza kazi yake ya uigizaji tokea miaka ya themanini akiwa chini ya mwalimu wake wa Suday School kwa jina James Odhiambo. Baadaye kwenye dhoruba za miaka ya tisini hadi elfu mbili akapitia kwenye mikono ya walimu waliobobea kwenye tasinia hii ya burudani ya uigizaji wakiwemo Daudi Mbogori na Yusuf Dalu. Baadaye tena katika miaka yake ya awali ya shule ya msingi akiwa mwanachama wa drama aliweza kunolewa katika mikono  ya Madama Catherine na Okumu Clifford.


Leon akifanya yake.
Hata hivyo safari hii haikuishia hapo kwani Leon amejikuta akiogolea kwenye dumbwi la sanaa, na kujiunga na vikundi mbalimbali vya sanaa ya uigizaji ikiwemo Kizingo arts troope, SAFE Pwani na baadaye akajiunga na Ashiner Pictures mwaka wa 2006. Kufikia hapa ndipo ndoto yake ya kuwa nyota wa filmu ilianza kuchukua uhai, maana aliigiza kwenye filamu tofauti ikiwemo Cheche, Sumu, Tandu na nyingine nyingi tu. Alitoka katika kampuni ya filamu ya Ashners nakuenda kucheza filamu ya Nyanya Rukia iliyokua ikiongozwa na muongozaji maarufu wa filamu Bw. Gitaru a.k.a GK. Hatimaye mwaka jana 2018, wakati filamu ya Pete ilipotangaza nafasi alijikuta pia yumo ndani na akapata nafasi ya kucheza kwenye tamthilia hii kama Mbaru. Nasasa kwasasa yupo chini ya ungozi wa kampun ya filamu ya AR chini ya inayoendeshwa muongozaji wa filamu Bw David Okello.

Taarifa imetayarishwa na Yusuf Dalu, kunakiliwa na kuandikwa  Changez Ndzai

Post a Comment

Previous Post Next Post