Bi Celestine Nyaga (NURU) msanii katika tamthilia ya Pete!
Celestine Nyaga anaigiza kama Nuru. Pete ni mchezo wake kama wa pili katika runinga. Ana tajriba kubwa ya uigizaji wa jukwaani. Binti mwenye nidhamu, mkakamavu na mwenye juhudi kubwa awapo kazini kwake.Ameigiza pia kwenye filamu ya OKOSOVO iliyochezwa Mombasa na kuonyeshwa kule Tanzania. Katika fani hii ya uigizaji amekua kama kioo ambacho kinatamalaki kwa nema ya mafanikio. Ukimtazama tu kwa umbali, umbo lake la wastaani, rangi yake na tabasamu isomuisha kwenye wajihi wake, kweli anakamilisha picha ama taswira kamili ya mwanadada mwenye ari ya kufikia malengo kama nyota wa kimataifa katika siku za usoni. 


Celestine akiwa kwenye ubora wake.
Mzaliwa wa Kwanza kwenye familia yao, na katika masomo yake ya upili alichambua vitabu katika shule ya upili ya wasichana ya Ngalla Memorial Girls iliyopo katika kauti ya Kilifi. Pia akiwa katika chuo cha masomo ya juu cha Technical University Of Mombasa (TUM), aliweza kutamba kwa weledi wake chuoni humu kama muigizaji kwenye tamthilia tofautitofauti. Na nikutokana na uwezo wake huu, ndio umemfanya mpaka sasa amepata fursa ya kuigiza kama Nuru kweye mchezo ama Tamuthilia hii ya Pete. Kupitia kalamu yangu hii, nakukaribisha shabiki wetu wa East Africa Bana kuweza kujivunia pamoja nasi usogora wa mastaa wetu kwenye kiwanda cha uigizaji Kenya, ambacho kinakua kila uchao.

Makala: Yamehakikishwa na Yusuf Dalu, kuhaririwa na kunakilawa na Changez NdzaiPost a Comment

Previous Post Next Post