Marapa wakali wa hapa nchini Kenya Monsta na K-Mode wameuanza mwaka mpya kwa njia ya kipekee. Hii ni baada ya kuingia studio na kutayarishia mashabiki wao kibao bomba kwa jina The Base, ambacho tayari kinafanya vizuri. Ikizingatiwa kuwa marapa hawa wawili ni miongoni ya wasanii wachache wanao fanya muziki wa kufoka hapa nchini ambao wamebaki kwani wengi wao wameingilia katika muziki ambao unafahamika na wengi kama wakubana pua. Hata hivyo licha ya kukubalika nawengi hapa Kenya pia Monsta anakubalika sana Tanzania haswa Arusha, Mwanza na Zanzibar ambapo radio kama Sunrise radio ya Arusha, Ice FM ya Mwanza na Swahiba FM ya Zanzibar. Video hii pia inatarajiwa kuonyeshwa rasmii kupitia kituo cha televisheni cha Y254 kwenye kipindi cha Ymashariki kinachoendeshwa na nahodha wa muziki wa kizazi kipya almaarufu kama Ken Rel Bis. Ngoma hii imepikwa kwenye studio za Beast mode Gang records na Zion, video ikang'amuliwa vilevile na Zion. Karibu mpendwa shabiki kuitazama ngoma hii.

Post a Comment

Previous Post Next Post