Ni mwanafunzi mwenye umri wa miaka kumi hivi katika shule ya msingi ya Bremma Academy iliyopo viungania mwa mji wa Mombasa katika ukanda wa Pwani ya Kenya na kwasasa yupo darasa la tano. Tayari anainuka na muinuko wa kipekee, kwakua na uwezo wa kuigiza kwenye tamthilia kubwa kama Pete. Alianza kuiga akiwa na umri wa miaka miwili, pindi tu wazazi wake walipogundua kuwa mtoto wao wa Kwanza anauwezo huu, walianza kukipalilia kipaji chake kwa hali na mali ilimrudai kumfanya malaika huyu mchanga wa filamu kuwa anatimiza ndoto yake ya uigizaji, na ndiposa kwasasa nyota huyu kinda anawaburudisha wengi si Africa Mashariki pekee bali Africa nzima kupitia tamthilia hii yenye kusisimua ya Pete.

Tayari akiwa na umri huu mdogo, ameweza kujipatia si umaarufu tu pekee, bali hadi kujiingizia kipato  cha haja kwani kupitia kampuni ya Mombasa Maize Millers nyota huyu alihusika kikamilifu katika kutengeneza matangazo ya kibishara ya kampuni hiyo. Na nikupitia tangazo hilo lilimfanya kutafutwa na uongozi wa tamthilia hii ya Pete na kujumuishwa ndani nasasa anaiga kama mtoto Sitara katika mchezo mzima huu wa Tamthilia inayosifika na hata kuangaziwa na vyombo vya habari vya kimataifa kama V.O.A (Voice Of America) nasasa nimiongoni mwa kundi la wasanii wa kuiga tendeti linalo iwakilisha nchi ya Kenya na Africa Mashariki kwa ujumla ndani na nje ya Bara la Africa. 

Taarifa imetayarishwa na Yusuf Dalu na kuhaririwa na kuchapishwa na Changez Ndzai.

Post a Comment

Previous Post Next Post