Anawezakana kuwa mgeni kwa wengi haswa kwakuwa jina lake halijatajika kama nyota wengine wa fillamu nchini Kenya,  ila Mzee Msiri kama anavyojulikana kwenye tamthilia ya Pete nimiongoni mwa watu muhimu sana nawenye tajriba na heshima ya kipekee kwani amekua kama mzazi wa mastaa wengi haswa kwa wale waliopitia ukumbi wa maonyesho ya sanaa mjini Mombasa maarufu kama Little theater. Ni miongoni mwa watu wachache waliokuwepo wakati Club hii ya maonyesho ya kuigiza ilipokuwa inafifia, na alihusika pakubwa sana kuikomboa kutokana na kutokomea kwenye kaburi lasahau. Gillie Owino mchango wake katika club hii ya little theater unaturudisha nyuma kiwakati hadi mwaka wa 1984, ambapo ndipo alipojiunga nakuwa mwanachama wa kikundi ama club hii ya sanaa ya maigizo. Nakupitia hapa, alijijengea heshima akiwemo kwenye vyeo mbalimbali kama (HHon Treasurer) mwaka wa 1989-1991, (LTC Commettee) 2014-2015, (Mombasa Carnival) 2013-2015, Kisiwa Fesstival -2016, (Author LTC Business) na nyingine nyingi.

Mzee Gillie Owino akiwa kwenye ubora wake.


Akiwa anaumri wa miaka 60, kwasasa amekamilisha ndoto zake zote kama Muandishi wa tamthilia, Muimbaji, muigizaji, muandishi wa vitabu mbalimbali na hulka nyinginezo ambazo wasanii wengi wangetamani kuzifikia. Katika maisha yake kwa ajili ya bidii na msisimuko wake kwenye sanaa, nyota huyu wa filamu ameweza kujizolea tuzo zenye heshima ndani ya Kenya, zikiwemo tuzo za Sanaa Awards mwaka wa 2018, Gillie amejaliwa na mke mmoja ambaye pamoja wamefanikiwa kupata baraka za watoto watano wakiwemo wavulana watatu na wasichana wawili. Kwamengi zaidi kumuhusu zidi kufatilia tamthilia ya Pete, nauweze kupata burudani zaidi kutoka kwa Mzee Msiri.

Mzee Gillie Owino (Katikati) akiwa na mwenzake wakihojiwa na mcheshi maarufu Africa Eric Omondi.


Makala yametayarishwa na Yusuf Dalu, kuhaririwa na kuandikwa na Changez Ndzai.

Post a Comment

Previous Post Next Post