PAPA JONEZ
Kwa mara nyingi wapenzi wa muziki wa kizazi kipya huwa wanapenda kufatilia nondo tamu zenye nyuga za kuvutia na kutia moyo. Haswa pale wanapomuona msanii anatoka chini kabisa na kung'ang'ana hadi kufikia hatua ya kuwa nyota wakimataifa. Msanii Kalighraph Jones ni mmoja wa baadhi wasanii ambao wamepitia hali hii. Basi kinacho wafurahisha wengi kwasasa, niile hatua aliyoichukua jana pale alipomchukua msanii wa Nigeria Iam Rudy Boy wa kundi lazamani la muziki PSquare hadi Kayole mtaa aliokulia na kumuonyesha sehemu tofautitofauti ambazo alikulia ikiwemo mahali alipofanya kazi ya kukaranga chapati kwenye kibada kimoja viungani mwa Kayole.Kwa hatua hii wengi wameichukulia kwa moyo mmoja na kumpongeza staa huyu wa hapa nchini Kenya. Mashabiki ama wafuasi wake wamemumiminia sifa zote huku wakihoji kwamba sirahisi kwa mastaa wa hadhi yake aliyofikia kukubali hali ngumu walioyopitia zamani, mpka kufikia hatua ya kuwakaribisha mastaa wenziwao nakuwaonyesha mahali duni walipotokea. Kaligraph pia alizuru shule yake aliyosomea, nakumpeleka huko mgeni wake Rudy Boy Square. Ukumbuke huyu Rude Boy Square si msanii tu hivihivi, ni mmoja kati ya mastaa ambao show zao ni ghali sana kuingia na kwa umaarufu alionao wote pia alikubali kushikana guu mosi guu pili hadi Kayole na Papa Jones ilikufanikisha ziara hii ambayo wengi wamedai kuwa inafaa kufanywaa kuwa Dokumentari kwa jinsi inavyovutia na kuhamasisha na kupeana changamoto kwa vijana wenzake kuwa kila wanapo tia bidii basi mwisho wa siku watajipata pahali pazuri kwa siku za usoni. Tayari kupitia maoni ya waliochangia kwenye video hii iliyopandishwa kwenye channel ya Coke Studio, wengi wamemukubali Papa Jones kwa kitendo hiki, lakini pia hawaja muacha Rudy Boy bila hongera kwani pia yeye alipitia maisha kama haya kabla ya kuinuka wakiwa pamoja na kakake wakati wakiwa kwenye kundi la muziki la PSqure kabla ya kuvunjika.

RUDE BOY 


Post a Comment

Previous Post Next Post