Kwa Tanzania jina Meena Ally, ni moja kati ya majina tajika na lenye uzani usiopingika mwazo mwisho. Kwanza kabisa keti kitako nikudokolea utandu si wa ubwabwa wala makombo ya biriani ila kwa uhundo ulionogewa ukakolea burudani lisilo na kifani. Mwanadada huyu anafahamika kwa mengi sana, tukianza na kazi yake kama mwanaharakati anayepigania haki za vijana wenzake na kinamamaTanzania. Kupitia taaluma yake ya uanahabari, nyota huyu wa Tanzania, amekuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha anawakilisha vyema maswala ya kupinga ukiritimba unaofanyiwa wakinamama na vijana nchini mwake. Natokea mwaka wa 2015, Meena amekua akifanya kazi na shirika la habari la BBC katika kipengele kinacho wajibikia hoja za vijana kwa jina '' Niambie''. Kupitia kipindi hiki, Meeana amejitengenezea jina miongoni mwa rika la vijana wenzake nahata wazee Africa nakumfunya kuonekana kama mfanao wa kuigwa kwenye jamii.Mbali na BBC, Meena Ally pia kwa mjibu wa bidii na ari aliyonayo kwenye taaluma ya utangazaji, basi Mwenyezi Mungu amemujalia kupata neeama ya kutangazia kituo cha habari chenye ushawishi mkubwa barani Africa na cha tatu kwa wingi wa wasikilizaji/mashabiki maarufu kama Clouds Fm Media nchini Tanzania. Ambapo sako kwa bako na mtangazaji mwenza wa kiume anayesifika kuwa mtangaziji mwenye waafwasi wengi zaidi ndani ya nchi ya Tanzania si mwengine bali ni Millard Ayo wamekua mstari wa mbele kuwa burudisha na kuwaongoa mashabiki wengi siku baada ya nyingine. Magwiji hawa wawili wanajikusanyia maaelfu na kuwafikia mamilioni ya wasikilizaji kila siku ya wiki kupitia kipindi chao maarufu cha Amplifaya ndani ya Tanzania na zaidi hadi nje ya Africa Mshariki shukrani kwa huduma za utandawazi.

Meena Akiwa na mtangazaji mwenza Millard Ayo


Meena Ally akihoji Mswada wa vyombo vya habari kwenye video hii.


Hata hivyo nyota huyu wa Tanzania, ameanza kupenya nchini Kenya kupitia kituo cha Televisheni Y254 TV, ambapo anaripotia habari za burudani zinazovuma ndani ya Tanzania katika kipengele cha Dondoo kwenye kipindi cha burudani almaarufu kama Y-Mshariki kinacho ongozwa na mtangazaji wa habari za burudani anayekua kwa kasi Africa Mashariki KenRelBis. Ukwasi wake kwenye mambo ya burudani, kumempa motisha wakufanya makubwa zaidi ndani ya Kenya na kupitia hamu ama motisha hii imemfanya kukataa kutia kikomo ama kotosheka na Y254 TV pekee bali Meena Ally pia anabisha na kutisha kwa kuwaburudisha na kuwaongoa wengi Kenya kupitia kituo cha radio cha Bahari fm kwenye kipindi cha burudani ya muziki wa kisasa maarufu kama Chachawiza.

Meena Ally akiwa katika pozi lake 


Ukumbeke kuwa Meena Ally mbali nakuwa mtangazaji, yeye pia ni mjasiriamali. Umaarufu wake haujamuacha mwanadada huyu kikapu kikavu. Chambilecho wahenga mgaagaa na upwa hali wali mkavu. Akiwa na takribani mashabiki laki mbili na hamsini katika kifurushi chake cha Instagram, Meena Ally amekua kivutio cha makapuni makubwa ambayo yameweza kutumia ukubwa wa wafuaasi wake kupitisha matangazo yao ya kibishara, kitu ambacho kinamfanya kuingiza kipato kizuri cha hela kwa kutangazia makapuni haya bidhaa zao. Makapuni haya ikiwemo Tigo Tz mwaka jana 2018 na Tecno Mobile. Nyota yake pia ya uanahabari imezidi kung'aa na hatimae kujumuishwa kwenye (Bongo Star Search), kitengo maalumu kinacho tumika Tanzania kuwasaka vijana wenye talanta na kuwasukuma ilikutambulika kwenye jamii na kupata ajira kupitia talanta zao. Usisahau kuwa Meeana Ally ashawahi kufanya kazi kwenye Televisheni nakuendesha vipindi kadhaa maarufu Tanzania kama ''Uswazi'' akiwa katika kituo cha televisheni cha East Africa TV.


Video ukimuonyesha Meena Ally kwenye tangazo la Tigo Fiesta mwaka jana.

Picha zaidi.


Bango likionesha tangazo la (Nambie)

Picha ikionyesha Meena Ali akiwa kwenye ofisi za BBC

Post a Comment

Previous Post Next Post