Mdau wa muziki wa burudani Mzazi Willy M Tuva akiwa na rappa mkali Africa kwasasa kutoka Kenya King Kaka.Sanaa nikitu muhimu na njia moja mbadala inayoweza tumika mbashara kwenye jamii kama kitega uchumi na kutoa ajira kwa vijana kwenye nchi husika. Lakini pia kama ajira nyingine ile, sanaa inahitaji mfumo fulani hivi kwa lugha ya kimombo (Dicipline) ama kwa kutohoa tu tukaita disiplini. Nikitumia mfano wangu mimi mwenyewe binafsi kama msanii wa uandishi wa habari za burudani, malenga na mhariri wa majarida mbalimbali ya habari za burudani mbali na kuwa ripota wa habari wa vituo vya redio ndani ya Kenya na nje ikiwemo radio Sunrise 94.9 FM Arusha Tanzania na mikoa mingine, SnS (Simulizi Na Sauti) yenye makao makuu jijini Dar Es Saalam, DizzimOnline Tanzania inayomilikiwa na Sallam Sk meneja wa kimataifa wa msanii Diamond Platnamz na vituo vingi vinginevyo tu vya kimataifa.

Moja kati ya makala niliyoyaandika kwa minajili ya kuwatangaza wasanii wa Kenya Tanzania nikiwa Bongo5 kama muandishi huru.Je nimewezaje kufanya kazi na media nyingi kwa wakati mmoja natena zingine zipo nje ya nchi? Swali hili ndilo linatupeleka hadi hatua ya kwanza, kwanini muziki wakenya unakwama kuvuka mipaka.

1. MAWASILIANO!

Mzazi Willy M Tuva jana aliuliza swali lili hili kupitia ukurasa wake wa mtandao wakijamii wa Facebook. Na mashabiki wengi basi wakatoa maoni yakwao. Ila mimi nitajibu kwanza kama mdau wa habari za burudani na mchanganuzi wa maswala ya burudani Africa Mashariki kisha tena kama muandishi wa habari za burudani/ ripota wa vituo vya redio kadhaa Africa Mashariki ikiwemo hapa Kenya na Tanzania. Mawasiliaono ni jambo muhimu katika maisha, uwepo wa mawasiliano mazuri baiina ya pande mbili za watu urafiki mzuri hujengeka. Hivyo msanii anapotengeneza mawasiliano mazuri na wadau tofautitofauti wa burudani, basi anaweza pata fursa yakufanya vyema kwenye ulingo wa burudani ndani na hata nje ya mipaka ya Kenya.

Kivipi? Je unajua asilimia kubwa ya watangazaji wa habari huwa marafiki? Basi unapojenga urafiki thabiti na mmoja wao anakupa nafasi ya kwanza kukutanisha na wanahabari wengine hivyo msanii unapata fursa ya kufanya interbiews kwa redio na runinga kwa urahisi, haraka na ufasaha. Mfano uliohai picha iliyopo chini ilipigwa mwaka jana Disemba maaeneo ya Karen nikiwa na Mzazi Tuva wa redio/Tv Citizen, Ken Rel Bis wa Y254TV na Presenta Ali wa Switch TV tukiwa katika mchakato mzima wa kuongea kwa kina maswala ya burudani. Wasanii wengi wa nchini Kenya wanafeli sana kuliweka akilini wazo hili la kuwa na mawasiliano bora na wadau wa burudani. Anapopata fursa ya kutambulika na kuukumbatia umaarufu, hua anamea nundu nakuwaona baadhi ya wadau wa burudani waliohusika pakubwa kumuinua kana kwa ni bure kabisa na hukatiza mawasiliano kwa kuonyesha dharau. Inapofikia hapa ndipo unaona msanii mara ghafla nashushwa chati kwa kunyimwa (airplay) na wasanii wapya kupandishwa badala yake. Je unafikiri msanii akifikia hatua hii ataweza kupenya nje ya mipaka ya Kenya kama nyumbani ameshushwa? Tafakari!

Nikiwa na wadau wa Burudani wenzangu Mzazi Tuva(Citizen radio/TV), Ken Rel Bis (Y254TV) na Presenter Ali (Switch Tv).


2. KIBURI/KIBRI!

Kiburi hakijengi na wala hakiwezi jenga mja hata nafasi moja maishani. Kiburi ni sumu kali haswa katika nyanja ya maswala ya burudani. Na kiburi kimeangusha wengi baadhhi ya watu maarufu duniania akiwemo mwana masumbwi wa nchni Marekani Mike Tyson. Wasanii wengi wanapopata fursa ya kuzitawala chati za redio mbalimbali Kenya, huanza kujiona wao ni nyota kuliko watu wengine wakiwemo hata wadau wa burudani ambao hao ndio wanahusika pakubwa kuwafanya wafike pale juu. Mtu kama mimi, ninao uwezo wa kuandikia tovuti mbalimbali za habari za burdani maarufu na kubwa Africa Mashariki mfano nishawahi kuandikia Bongo5 kipindi ambacho msanii Diamond Platnumz alikua anainuka. Na blog ya Bongo5 Tz chini ya Dr. Fredrick Bundala wakati huo, maana  kwasasa yupo SnS TZ Media (Anayoimiliki mwenyewe), ilihusika asalimia 99.5 kumutangaza Diamond Platnumz kwa kuangazia kwa kina kila alichokifanya siku baada ya siku. Namimi nikiwa mmoja ya waandishi wa kuhusishwa nakumbuka niliandika baadhi ya makala ya kumjenga Diamond alimradi afikie malengo yake na ndoto zake katika kuupeleka muziki wake juu. Hatimae kwakua Diamond alijali na kuheshimu waandishi wote wa habari na hana kiburi, leo hii amefanikiwa kufungua kituo chake mwenye cha habari.

Moja kati kazi zangu nilizoziandika kupitia Bongo5 kuhusu Diamond Platnumz kama muandishi huru chini ya uongozi wa Dr. Fredrick Bundala.


Je kama niko na fursa ya kuandikia na kuripotia vituao vya habari kama Bongo5 Dar, DizzimOnline Dar, Sunrise radio Arusha, Jembe FM Mwanza, Swahiba FM Zanzibari, Ice FM Njombe Tanzania navingine vingi. Je nikitu gani kitazuia uwezo wakupeleka kazi za wasanii wetu wa Kenya kwenye vyombo hivi vya habari vya nchini Tanzania nazisichuliwe? Uhusiano wangu na baaina ya wadau wakuu wanao sambaza kazi za wasanii kwenye media tofauti Africa Mashariki ni mkubwa na simimi pekee kama nilivyotangulia kusema, watangazaji na MaDj wengi Kenya wanazo chaneli (Chanels) zakuwa sukuma wanamuziki wetu si hapa Africa Mashariki pekee bali hadi Nigeria na Africa Kusini ila viburi vimekwamisha kabisa hatua hii nakuwafanya wadau wengi kuwabania kwa kufungia wasanii fulani na kuwapanndisha juu wengine wapya kila uchao na hapa ndipo tunapata muziki wetu wa Kenya unazidi kudorora kila uchao. Wasanii waanze kujirudi na kuweka kwenye akili kuwa muziki ni ajira ila si njia ya kuuza suura ama kujipatia umaarufu. Tengeneza bishara yako kwa kujenga brandi yako kupitia muziki, pata pesa, jijenge umaarufu bado utakufuata. Chukua maamuzi Mapya!


Baadhi ya kazi zangu ndani ya Bongo5 Tanzania, niya yangu kuu kutangaza kazi za wakenya wenzangu.


3. MAUZO!

Naamini kila bishara nilazima iwe na mtaji (Capital), hivyo muziki pia kama biashara nyingine inahitaji mtu ama msanii aweke hili kwenye akali. Waandishi wa habari na wadau wa maswala ya habari za burudani ni wengi sana, nawapo mara mbili. Kunawengine wameajiriwa na vyombo husika vya habari na kuna wengine ni wakujitegemea kwa kimombo tunawaita (Freelancers). Msanii anatakiwa kubainisha na kuwa na uwezo wa kutofautisha kati ya makundi haya mawili. Mfano uliohai, Babu Tale kabla ya kuwa meneja wa Diamond Platnumz alijaribu kuingia muziki kama rappa akiwa pamoja na msanii Madee Ali. Ila alipogundua kuwa hawezi kuimba ama kuwa rappa, akaamua kuwa msambazaji wa kanda za muziki za mwenzake Madee kwenye media tofauti Tanzania na pia Kenya. Wasanii wa Bongo flava wakati huo walipoona nafasi ile, akiwemo Diamond wakati huo ndio mwanzo anainuka wakamfuata Babu Tale iliawezeeshe kuwasukumia muziki wa kwa vyombo vya habari Tanzania na Kenya pia Uganda kwakua alikua na connection.

Meneja mmoja wa mameneja anayehusika na maswala ya kiabishara ya ndani ya Tanzania wa msanii Diamond.


Babu Tale akakubali ila kwa sharti moja, kila msanii ilibidi alipishwe ama kutozwa ada flani hivi ilikuwezesha Tale kufanya huduma ile kwa moyo mmoja na safi. Hakuna aliyepinga na wasanii wote waliofata masharti yake ya kutoa ada kwa huduma ya kusambaziwa kazi zao za muziki kwenye media za Tanzania na nje wote walifanikiwa. Ninapoandika waraka huu mda huu kwasasa, Babu Tale yule mdau wa burudani wakusambaza muziki kwenye media wakati ule, sasa ni meneja tajika na anaheshma na taadhima ndani na nje ya mipaka ya Tanzania. Naamanisha hivi, msanii nilazima ujipange unapoingia kwenye muziki. Ujue muziki umebadilika siku hizi, kutoka (Hobby) hadi kuwa biashara. Nakama mwanabishara, msanii unafaa kujipanga jinsi utakavyousambaza muziki wako ndani na nje ya nchi ya Kenya. Unapowekeza vizuri katika kuusukuma muziki wako, basi utajikuta unavuna mavuno mazuri. Ila unapotegemea miujiza kufanyika kwa kulala na kuota, utafulia madafu ya mkwezi. Kumbuka si wadau wote wanavigezo hivi, ama fursa hii. Utapata hapa Kenya kwasasa nikidogo sana, hivyo msanii unapopata mdau huru na anatoza ada, unafaa uzingatie unufaike kwani wadau huru huwa wanatumia nguvu zao wenyewe kusukuma muziki wako kwa media, tofauti na wadau walioajiriwa. Sasa msanii huoni haya ama huruma mtu anapojitolea kukupa viunganishi kwa  hiyari yake mwenyewe pengine kukupelekea muziki wako kwa radio, runinga ama uandikwe kwenye tovuti maarufu za burudani, unachotka kazi hii niaifanye bure bilashi?  Jamii yake itakula nini na atalipa vipi kodi ya nyumba na mahitaji mengine? Namaliza kwa kusema ukiyavulia nguo sharti uyaoge.Msanii amua mwenyewe!

Mtaarufu wa makala haya sikuvunja moyo wasanii, bali kuwapa changamoto waanze kutazama kazi ya usanii kwa jicho la tatu!
Post a Comment

Previous Post Next Post