Akothee akiwa ofisini mwake
Kawaida ya hulka ya kila binadamu nikufurahia pindi aonapo mwenziwe anapatashida. Binadamu tumekuwa na mazoea ya kuongelea matatizo na kushangilia wenzetu wanapopata shida haswa ikiwa muhusika anauwezo na umaarufu unao pitiliza. Mwanamuziki na mjasiriamali Akothee ni mfano wakupigiwa upato kwahili. Kwani amekua akigonga vichwa vya habari Africa Mashariki kila uchao kwa matukio ya kwake ambayo kwa mara nyingi wengi humukemea kwa kudai anapitiliza mipaka, na kwa vitendo vyake hivyo anakeuka maadili na mienendo kinyume na tamaduni zetu za kiafrica.

Kinacho shangaza zaidi asilimia tisini na tano ya watu ambao huwa wanamukashifu Akothee, wao nao pia utawakuta wamo kenye kundi lilohilo chambilecho wamombo walipo sema ''Are sailing in the same boat'' Kwamaana kwamba wanasafiria kwenye bahari wakitumia mwau uleule. Tofauti ya Akothee na wale huwa wakwanza kumukemea, huwa ni yeye Akothe ni maarufu ila hao wamo nyuma ya pazia. Hivyo ulimwengu hauwezi kuwaona, kinyume na Akothee ambaye ni maarufu na anamulikwa kwa kina haswa na vyombo tofauti vya habari vya humu nchini na hata vya kimataifa.

Jinsi Akothee alivyopokelewa wakati akizuru Lodwar, katika mchakato mzima wakusaidia wahanga wanjaa.


Jumamosi hii ya leo ya tarehe ishirini na tatu mwezi ukiwa ni wa machi, mwanamuziki huyu nguli wa hapa kwetu nchini Kenya, amewanyamazisha wapinzani, hasimu, adui zake na kadhaalika kwa kufikisha chakula cha msaada katika Kauti ya Turkana ambayo imekuwa ikitawala vyombo tofauti vya habari kote nchini kwa kukumbwa na baa la njaa licha ya serekali yenyewe kupinga kuwepo na tatizo hilo la njaa. Akothee akiandamana na meneja wake Nelly, na wahisani tofauti amefikisha ahadi yak kwake aliyoiweka mwaanzoni mwa juma hili. Hata hivyo tofauti ama kinyume na vile jina lake hu trendi kwenye mitandao mingi ya kijamii wakati anapofanya vituko vyake kwa ajili ya burudani, Kwasasa wengi wamefyata midomo huku bumbuazi ikiwa imewakuta chambile Yonda lililo fumaniwa liwkiwa katika harakati ya kuiba mahindi kwenye Konde la wenyewe. Hata hivyo Akothee lich ya chuki kutoka kwa mahasimu wake, ameonekana kutojali na anapiga soga zake za kutafuta shilingi siku baada ya nyingine bila ila. Je unafikiria huu ndio mwazo wa Akothee kuanza kuwashangaza adui zake kwa mema mengi anayoyafanya ila wengi wamekaznia kwa vituko vyake vichache tena sababu ya burudani? Usilijubu swali hili endelea tu kutegea kwa mwasho zaidi wa habari za burudani kutoka kwa meza yetu ya habari. Tazama picha zaidi hapa chini.
Post a Comment

Previous Post Next Post