Sister Shaniez...Mtangazaji


Baada ya wiki kadhaa za ati ati kuhusu ujio wa kituo kipya cha radio ukanda wa pwani chini ya mwavuli wa kampuni ya Mediamax, hatimaye mipango inaonekana imekamilika na kitazinduliwa siku ya Jumatatu.
Hata hivyo, kinyume na wengi walivyotarajia, kituo hicho kimezinduliwa na jina jipya jengine “MsenanguFm” mbali na la awali la “AsenaFm”  lililokua likivumishwa mitandaoni.
Mapema leo kituo hicho kimeanza kupeperusha ratba ya vipindi pamoja na vitambulisho vipya vya stesheni hiyo, huku tarehe rasmi ya kuanza kuwaskia watangazaji hewani ikitangazwa kuwa ni jumatatu hii ya tarehe 20/05/19.
Kulingana na taarifa za ndani tulizozipata, kampuni hiyo ilifanya maksudi kutoa jina la uongo mwanzoni ili kuwazuga maadui wa kibiashara ambao inaripotiwa hawajatulia tangu mipango ya kuzinduliwa kituo kipya kufichuka.
Inasemekana vita vya kibashara vilianza pindi tu Mediamax ilipotangaza kuibadili Pilipili Fm kuwa kituo kinacholenga jamii ya wamijikenda na wa pwani kwa ujumla kipya
Kituo hicho  kimesheheni watangazji kutoka vituo vya Radio Kaya na Pwani Fm ambapo kitapepereusha matangazo yake kwa lugha ya Kimijikenda na Kiswahili kupitia masafa ya 99.5Fm Mombasa, 101.0Fm Kilifi, 94.7Fm Lamu na 102.1Fm Voi
Watangazji hao ni Pyukapyu Wa Pyukupu(PPO), Sister Shaniez (AntiVirus), Fatuma Mwangala (TotoBomba,) Bahati Ngazi (MtotoRangiYaPesa)Teddy Mwanamgambo(BaloziWaChipkizi) kutoka Radio Kaya, Gaspery Tumaini (KabathaKalume) Josephine Medza (GomaRaKanani) kutoka Pwani FM na Ian Mtoti Mgalla(IMM)


Post a Comment

Previous Post Next Post